Wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wapewa onyo kuacha kushindana wenyewe kwa wenyewe.

WAKUU wa Wilaya  na Wakurugenzi Watendaji  wameonywa kuacha kushindana  wenyewe kwa wenyewe,  na kuendeleza migongano badala isiyo na tija  badala yake  washirikiane kwa kuwa  wanategemeana , katika kutekeleza  Majukumu yao.
Onyo hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene mjini Dodoma jana wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi hao wa mikoa sita kutoka Kanda ya Ziwa.
Simbachawene  amewataka wachukuliane hali, hisia, tabia na wavumiliane na kushirikiana ,badala ya kuonesheana ubabe na kila mmoja kujiona ana madaraka kuliko mwenzie.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mussa Iyombe amewataka  viongozi  hao kujifunza kwa bidii katika semina hiyo, kujua vizuri  Majukumu yao na Mipaka ya kazi yao badala ya kukaa siku tano na kurudi watupu.
Mafunzo hayo  yamewashirikisha  viongozi kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Simiyu, Manyara na Geita,
Exit mobile version