Walemavu watakiwa kuendelezwa kimasomo

AFISA miradi ya Elimu Jumuishi kutoka kitengo cha Kanisa la Free Pentecostal of Tanzania (FPCT) wilaya ya Dodoma na Bahi,Jane Mgidange amewashauri wazazi na walezi kutozimisha ndoto za watoto wenye ulemavu walizokuwanazo kwa kushindwa kuwaendeleza kimasomo zaidi.

Mgidange amesema hayo alipokuwa akizungumza na wazazi na walezi ambao familia zao zina watoto wenye ulemavu wanaosoma waishio katika kata ya Nkuhungu jijini Dodoma.

Alisema watoto wenye ulemavu wana haki ya kimsingi ya kuendelezwa ndoto zao kimasomo badala ya kuwaficha na kuwaweka majumbani.

Alisema kuna baadhi ya wazazi na walezi hawana moyo wa kuwaendeleza watoto hao wenye ulemavu,kwa imani kuwa hawawezi kutoa mchango wowote kwenye jamii wanayoishi nazo suala ambalo ni upofu wa kifikra.

“Changamoto iliyopo kwa wazazi na walezi wenye watoto ambao ni walemavu,wanawaona watoto hao kama ni sehemu ya mkosi hivyo hakuna haja yoyote ya kuwaelimisha kimasomo japo kuwa wengine wana vipawa”alisema.

Akizungumza na familia hizo pia ameziomba kuendelea kutoa elimu ya kujilinda na corina kwa jamii wanazoishinazo hata Kama ugonjwa huo umetoweka kama ilivyotangazwa na serikali.

Kwa upande wake Recho Lauret (11) ambaye ni mlemavu wa viungo mwanafunzi wa darasa la 5 shule ya msingi Nkuhungu Dodoma,alisema kuwa changamoto waliyonayo ni ukosefu wa vifàa rafiki visaidizi ikiwemo kutembea kwa mwendo mrefu wa kwenda shuleni.

Recho àlisema kuwa kutokana na ukosefu huo wa vifàa rafiki inawafanya walemavu walio wengi kushindwa kufikia ndoto zao pamoja kama ilivyo kwa wengine ambao hawana ulemavu.

Naye msaidizi wa mkuu wa shule ya msingi Nkuhungu jiji la Dodoma Rogathe Makupa àkizungumza kwa niaba ya wazazi na walezi ambao wana watoto wanaosoma shuleni hapo.

Alisema kuwa vifaa vilivyotolewa na taasisi ya Kanisa la FPCT kwa kushirikina na kituo cha habari kuhusu ulemavu ikiwa chini ya udhamini wa shirika la International Aid Services (AID) toka Denimark.
Vimetolewa kwa malengo ya kuwasaidia wanafunzi hao wenye ulemavu kuwa muda wote wanakuwa wasafi ukizingatia kuwa walio wengi wana ulemavu wa viungo

Makupa alitaja vifaa vilivyotolewa ni pamoja na ndoo,sabuni,vitakasa mikono na barakoa,vyote hivyo vikiwa na lengo la kuwalinda watoto hao wakiwa majumbani mwao na maambukizi ya corona pamoja na ugonjwa huo umeshatoweka hapa nchini kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali yetu.
Mwisho.

Exit mobile version