Wamachinga wametakiwa kwenda kuchukua vitambulisho vipya

Wajasiriamali wadogo jijini Arusha maarufu kama wamachinga wametakiwa kwenda kuchukua vitambulisho vipya vya awamu ya pili ili kuweza kuepukana na changamoto ya kufukuzwa na askari migambo kwenye sehemu zao za kazi

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa mtendaji wa kata ya Olorien Nemes Matem amesema kuwa  kata hivyo imeshaanza mchakato wa mtaa kwa myaa katika kuhakikisha kila mjasiriamali mdogo anapata kwa wakati ili aweze kuendelea na biashara zao

Amesma kuwa, vitambulisho hivyo vina faida kubwa ikiwa ni pamoja na wajasiriamali kufanya biashara zao kwa uhuru, na kuweza kuipatia nchi kipato wakati Rais akiendelea kusisitiza juu ya Tanzania ya viwanda

Hata hivyo amewataka wafanyabiashara kuachana na mambo ya siasa na badala yake wavilipie kwa wakati na kuendelea na biashara zao

Exit mobile version