Wananchi wilayani Kilindi mkoani Tanga,wameiomba serikali
kuharakisha mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango Cha lami
kutoka Handeni hadi kiteto mkoani Manyara Ili kurahisisha
shughuli za kiuchumi ikiwemo usafirishaji wa mazao.
Rai hiyo wameitoa wakati Makamu wa pili wa Rais wa serikali
ya mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdula,alipowasili
kwa ajili ya mkutano wake na viongozi mbalimbali wa kichama
na serikali.
