Wanachama wa mifuko ya jamii wametakiwa kulipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma zilizopo pasipo kuangali mfanyakazi ameacha au kuachishwa kazi.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa utekelezaji na usajili SSRA Lightness Mauki Katika mkutano wa baraza la 24 la wafanyakazi mkoani morogoro ambapo amesema kuwa sheria za mifuko ya jamii na utumishi wa umama zinatoa vigezo mmoja kwa moja namna mtu atakavyolipwa mafao baada kwa kuacha kazi mwenyewe ama kuachishwa kazi .
Akiongea wakati wa kufunga mkutano wa baraza hilo mkurugenzi msaidizi wa utawala wizara ya elimu Steven Pancras ameseama kuwa leno la serikali katika elimu ni kuhakikisha wanainua kiwango na ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi zote kuimalisha uwezo wan chi katika kuendeleza mafunzo ya sayansi na tecknolojia.
