WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

In Kitaifa

Na Tonie kaisoe ,Arusha

Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu mbalimbali za kudhibiti rushwa na kutojiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya ili watimize ndoto zao.

Akizungumzia lengo la kongamano Hilo la siku ya wanawake duniania lililofnyika katika chuo Cha uhasibu Arusha ,Ofisa Elimu Jamii kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini(DCEA) Shabani Miraji alisema mamlaka hiyo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Arusha wametoa elimu ya pamoja ili kuzuia wanafunzi wakike kutojiingiza katika matumizi ya dawa hizo pamoja na suala zima la rushwa.

Amesema utoaji elimu kwa wanafunzi hao umeenda sambamba na shuhuda za watumiaji wa dawa za kulevya wapatao 20 ambao walitoa elimu kwa wanafunzi hao wasiingie kwenye tamaa zitakazowapelekea kutotimiza ndoto zao hapo badae.

Amesema Baadhi ya wanawake wanapojiingiza katika matumizi ya dawa hizi na kuchelewa kupata tiba wanaathirika kiakili kutokana na maumbile yao Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii,Sarah Ndaba kutoka DCEA Kanda ya Kaskazini alisema wanawake ni walezi wanaotegemewa kuwa mama bora hapo badae Wakati huo huo,Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)Mkoa wa Arusha,Zawadi Ngailo alisema watoto wa kike lazima wapewe mbinu za kukataa rushwa zozote ikiwemo rushwa ya ngono na kutoa taarifa sehemu husika ili hatua zichukuliwe hivyo lazima rushwa isifumbuwe macho katika kudhibiti dawa za za kulevya nchini

mmoja kati ya waraibu aliyeacha dawa hizo, Susan Samwel alitoa rai kwa wanafunzi hao kuacha kutumia dawa hizo badala yake wasome kwa bidii huku akishukuru nyumba za kutolea matibabu (sober house) kuendelea kutoa huduma ili waweze kuwa wamama bora na kubuni miradi inayowakwamua kiuchumi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

MAJALIWA ATOA RAI KWA WAMILIKI WA MALORI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja

Read More...

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu