ZAIDI ya wanafunzi Elfu Thelathini 30,000 wa vyuo vya elimu ya juu nchini kwa mwaka mpya wa masomo 2017/18, watanufaika na Sh bilioni 427 kutoka Bodi Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), huku wanufaika hao wakiwekwa kwenye mikondo mitatu.
Akizungumza na Vyombo vya habari , Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul –Razaq Badru amesema kwa mwaka huu wanufaika wasiopungua elfu thelathini, watapata mikopo ya elimu kulingana na fani walizochagua kusoma.
Akifafanua idadi na kiwango cha mkopo kitakachotolewa kwa kila mkondo kulingana na fani watakazosoma, ambapo amesema bodi imepanga mikondo mitatu ya mikopo.
Mkondo wa kwanza utawahusu wanafunzi wa fani za afya, sayansi ya elimu na hesabu, ambapo kundi hilo litapata asilimia 40 ya mkopo huo ambao ni sawa na Sh bilioni 170.8.
Badru amesema kundi hilo ndilo litapata mkopo mkubwa kuliko makundi mengine kutokana na fani hizo kuwa adimu na zina mahitaji makubwa ya soko nchini hasa kwa kuwapata wataalamu watakaosaidia taifa kwenye sekta za afya, sayansi na elimu.
