HALI za wanafunzi majeruhi wa shule ya Lucy Vincent ya mkoani Arusha, waliopele kwa hospitaliya Mercy jijini Sioux katikajimbo la IOWA nchini Marekani kwa matibabu inaendelea vizuri na tayari wote watatu wamefanyiwa upasuaji.
Majeruhi SadyaAwadhna Wilson Tarimo wote walifanyiwa upasuaji jana wakati DorenMshana alifanyiwa juzi.
Mtu wa Karibu anayefuatilia afya za watoto hao na Mbunge wa Singida Kaskazini na rafiki wa karibu wa watalii madaktari waliowaokoa majeruhi na kuopoa maiti siku ya ajali Mei 6, mwakahuu.
Nyalandual amesema kuwa kila motto amewekwa kwenye chumba chake na mama yake pamoja na muuguzi mmoja.
Mbunge huyo alisema Sadya amefanyiwa upasuaji maeneo matatu yaliovunjika ikiwemo mkono wakulia lakini shingo haikufanyiwa upasuaji na badala yake aliwekewa kifaa cha kunyoosha (Brace) atakayokaanayo wiki sita kuanzia sasa.
