Wanafunzi watatu waliopata ajali wahudhuria masomo yao rasmi.

In Kitaifa

WANAFUNZI watatu waliopata ajali ya basi la Shule la Lucky Vincent ya jijini Arusha Mei mwaka huu katika eneo la Rhotia wilayani Karatu, wamehudhuria masomo yao darasani jana kwa mara nyingine huku wanafunzi wenzao wakifurahi.

Wanafunzi hao Sadya Awadhi, Wilson Tarimo na Doreen Elibariki, waliwasili kwa usafiri wa pamoja binafsi shuleni eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha,huku wakisindikizwa na wazazi wao.

Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Lucky Vincent, Longino Mkama, watoto hao waliwasili jana asubuhi, na walipofika walipokelewa na wanafunzi wenzao huku kila mmoja akishangilia hususan wanafunzi wa darasa la saba, waliokuwa wakisoma nao kabla ya kupata ajali iliyosababisha wapelekwe Marekani kwa matibabu zaidi.

Akizungumzia kuhusu watoto hao kutumia usafiri wa mabasi ya shule, amesema hawatatumia mabasi ya shule kwa kuwa, bado wana hofu na ajali, hivyo wazazi wao kwa pamoja wameamua kutumia usafiri wa magari binafsi kuwapeleka shuleni asubuhi kisha kuwarudisha majumbani mwao nyakati za jioni.

Juzi wazazi wa watoto hao walimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuwasaidia ili watoto wafanye mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

MAJALIWA ATOA RAI KWA WAMILIKI WA MALORI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja

Read More...

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu