Wanafunzi hao wa kidato cha sita wamefanya vurugu hizo usiku baada ya kutoroka shuleni, na kuvamia kwenye sherehe ya harusi ambapo wametaka sherehe hiyo iendelee hadi muda watakao amua wao.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani humo SACP Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Pia ameeleza kuwa wanafunzi hao 106 wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.