Wanafuzi 3 waliokua wakipata matibabu Marekani kurejea Nchini ijumaa.

Wanafunzi 3 wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent ya mkoani Arusha waliojeruhiwa katika ajali ya basi Mei 6 mwaka huu, wanatarajia kuwasili nchini Ijumaa kutoka nchini Marekani walikokuwa wakipata matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu,watoto hao wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa saa 3 asubuhi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA.

Wanafunzi hao ni Dorin Mshana, Sadia Awadhi na Wilson Tarimo, ambao walipelekwa nchini humo Mei 14 mwaka huu, kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mercy Medical iliyoko Sioux City.

Nyalandu ambaye ni mmoja wa waasisi wa Taasisi ya Stem iliyoratibu safari ya majeruhi hao kwenda Marekani, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuwapokea watoto hao ijumaa.

Exit mobile version