Wanajeshi 39 wa AU wadaiwa kuuawa na Al-shabaab

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali la Al Shabaab limedai kwamba limewauwa wanajeshi 39 wa kikosi cha Umoja wa Afrika baada ya kuwavamia katika jimbo la Lower Shabelle ingawa madai hayo hayajathibitishwa.

Wapiganaji hao wa Al Shabaab waliushtukiza msafara wa jeshi la Umoja wa Afrika umbali wa kilomita 150 kusini magharibi kutoka mji mkuu wa Mogadishu.

Kundi hilo la kigaidi linapigana ili kuwaondoa wanajeshi wa kulinda amani wa kikosi cha Umoja wa Afrika.

Vilevile wanataka kuing’oa serikali ya Somalia inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.

Umoja wa Afrika una wanajeshi wapatao elfu ishirini wanaopambana na Al Shabaab pamoja na kuiunga mkono serikali ya Somalia.

 

Exit mobile version