Wanamgambo wa misimamo mikali ya kidini wamefanya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya maafisa wa polisi wa Misri katika rasi ya kaskazini ya Sinai hapo jana, na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine 11.
Maafisa wamesema wanamgambo hao waliifyatulia risasi gari ya kijeshi kabla ya kuichoma moto katika mji wa el-Arish.
Vikosi vya usalama vilipowasili katika eneo hilo, wanamgambo hao walirusha bomu pembezoni mwa barabara.
Mapema jana, ndege za kivita za Misri za aina ya F-16 zilishambulia mikusanyiko ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo, katika maeneo kadhaa ya kaskazini mwa Sinai, na kuwauwa watu 30.
