Mkuu wa Wilaya akizungumza jambo katika studio za Radio5fm.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya akisalimiana na Mkurugenzi wa Radio5fm Ndugu Robert Francis
Afisa wa (NIDA) Bi.Julieth akisalimiana na Mkurugenzi wa Radio5fm Ndugu Roberth Francis.
Aidha amesema kuwa wananchi wasisubiri mpaka zoezi hilo kufikia tamati ndio kujitokeza Kwa wingi kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano na usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Naomba niwafahamishe na kutoa rai kwa wananchi wangu wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili na wasisibirie siku kubaki chache ndio wajitokeze kwa kuwa kunapelekea usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi”alisema fabian
Pia ametaka kila mwananchi kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala ya kisiasa kutokana na umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na kusajili na kutoa vitambulisho vya taifa.
Afisa kutoka mamlaka hiyo wilaya ya Arusha Mjini Juliette Raymond Amesema lengo la zoezi hilo ni kuwezesha serikali kutambua wananchi wake wapo wapi na wanafanya nini ilimradi anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania ,hivyo zoezi hilo ni lazima kwa kila mtu kwa Mujibu wa sheria.
Kwa wilaya ya Arusha Mjini zoezi hilo linaendelea katika kata ya Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi hilo linafnyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kata ya Sekei,Themi katika viwanja vya nane nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji kata eneo la Mbauda Sokoni.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Afisa wa (NIDA) katika Picha ya Pamoja na watangazaji wa Radio5fm.
