Wananchi mkoa wa Pwani wamehimizwa kushirikiana katika masuala ya kijamii, ikiwemo suala la usalama na kilimo cha matunda na zao la korosho na kuondokana na masuala ya migogoro ya wafugaji na wakulima, ambayo imekuwa ikigharimu maisha ya watu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alipokuwa akihitimisha ziara yake wilayani Kibaha, amesema kuwa mkoa wa Pwani una viwanda vitatu vikubwa vya kusindika matunda kwa sasa ambavyo endapo wakulima watavitumia watanufaika kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo katika hatua nyingine, Mhandisi Ndikilo amewaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kukimbilia kuwekeza mkoani Pwani kwani mkoa huo unaelekea kuwa ukanda wa viwanda na uwekezaji.
uishi kwa amani.
