Raia nchini Angola leo wameingia katika uchaguzi kwa kupiga kura ya kumchagua rais mpya wa taifa hilo.
Rais Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, na kuwa rais wa pili barani Afrika kuwa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi.
Rais Santos hawanii tena uchaguzi huu ambao waziri wa ulinzi Joao Lourenco, anawania kama mgombea kupitia chama tawala cha MPLA.
Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa Isias Samakuva, kutoka chama cha hasimu wa MPLA Unita.
Wachangazi wanasema kuwa chama cha MPLA ambacho kimekuwa madarakani tangua uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975, kinaonekana kuwa kitaibuka mshindi.
Baada ya vita Angola ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa na uchumi uliikua kwa haraka zaidi duniani, kutona na utajiri wake mkubwa wa mafuta.
Lakini wakati bei ya mafuta ilishuka miaka miwili iliyopita iliadhiri uchumi wote wan chi hiyo.
Ikiwa asimia kubwa ya watu wako chini ya umri wa maiak 35, hao ndio watakuwa na uamuzi mkubwa.
