Wananchi wa Mkoa wa Simiyu watakiwa kutumia vizuri fedha wanazozipata kwa mauzo ya pamba.

In Kitaifa

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Jimbo la Kisesa Wilayani Meatu mkoani Simiyu kutumia vizuri fedha wanazopata kwa kupitia mauzo ya pamba kununua chakula cha kutosha na kukihifadhi ili kuondokana na uhaba wa chakula.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwagayi Kata ya Itinje Wilaya ya Meatu, ambapo amesema kuwa uamuzi uliofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia ongezeko la bei ya pamba umelenga kuboresha maisha ya wananchi wanyonge waliodhulumiwa kwa miaka mingi.

Amesema kuwa Rais amesimamia msimamo usioyumba katika suala la pamba ambapo kwa sasa bei ya pamba imefikia shilingi 1200 kwa kilo tofauti na hapo awali ambapo wakulima walikuwa wakidhulumiwa kwa kulipwa shilingi 600 kwa kilo.

Aidha, Mpina amewataka wananchi hao kutumia mabadiliko hayo ya bei ya pamba kama fursa ya kuboresha maisha badala ya kutumia vibaya fedha hizo kwa mambo ya anasa ikiwemo kuongeza idadi ya wake.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. Magufuli ,imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi wanyonge na ndio sababu ya kuwekwa msimamo huo kuhusu bei ya pamba.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu