Wananchi wamelalamikia kiwango cha juu cha gharama za viingilio kwenye Maonesho ya 41 ya Bisahara ya Kimataifa ya Dar es salaam, maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa kwamba ni vikubwa ikilinganishwa na hali ya maisha ya wakati huu.
Wakizungumza na wanahabari wananchi hao wamesema gharama hiyo ya kiingilio cha juu cha shilingi 4000 za kitanzania ni kubwa ikilinganishwa na shilingi 2500 za mwaka jana, hali ambayo imesababisha wengi kutoweza kumudu kutokana na kile walichodai hali ngumu ya maisha iliyopo kwa sasa .
Baada ya Malalamiko hayo wanahabari walilifanikiwa kuzungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE ambao ndio waandaji wa Maonesho hayo.
Hata hivyo Kwa mujibu wa Tantrade, hakutakuwa na mabadiliko ya gharama kwa siku tano za nyongeza za maonesho hayo.
