Jeshi la Polisi katika mkoa wa Simiyu,limetoa wito kwa wale
wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria,kuhakikisha kuwa
wanazisalimia silaha hizo ndani ya muda waliopewa zikiwa
zimesali siku 19 tu.
Wito huo umetolewa na kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu
ACP Edith Swebe alipokuwa akizungumza na wanahabari na
kueleza kuwa,baada ya kipindi hicho kumalizika takayepatikana
na silaha kinyume cha sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi
yake.
