Wanaotaka kuendeleza Mapigano Sudan sasa waone aibu-Mamabolo

Kwa kuwa hali ya amani na usalama nchini Sudan imeanza kubadilika na kuwa nzuri, sasa ni wakati muafaka kwa pande zote kinzani kutumia fursa hiyo na kumaliza kabisa mzozo ulioanza nchini humo mwaka 2003.

 

Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, huko Darfur, UNAMID Jeremiah Mamabolo amesema hayo akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa akisema kuwa fursa ya sasa ni ya kipekee na haijawahi kutokea.

 

Amesema sitisho la mapigano linazingatiwa na wale wanaotaka kupigana wanapaswa kuona aibu kwa kuwa mazingira muafaka ya kumaliza mzozo huo ni pamoja na …

 

“Kuondolewa kwa vikwazo kulikofanywa na Marekani, na maazimio chanya kutoka mkutano wa viongozi wa Muungano wa Afrika kuhusu Sudan na ukanda mzima ambapo watu wanawatakia mema wasudan. Hivyo basi wao wenyewe wanatakiwa kutambua hilo na kumaliza machungu haya ambayo yamewafika wananchi kutokana na vita hivi.”

Exit mobile version