Wanawake wajitosa kuosha magari Arusha

In Kitaifa

Baadhi ya vijana wa kike na wa kiume jijini Arusha wamejitoa kwenye makundi ya mtaani na kufanya kazi ya kuosha magari maarufu kama car wash ili waweze kujikwamua kimaisha

Walizungumza na vyombo vya habari wakati walipotembelewa kwenye kituo cha uptown carwash vijana hao wamesema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya kupata ajira na hii inatokana na vijana wengi kuchagua kazi na kuwa wavivu wa kufanya kazi

Kwa upande wake mwanadada Neema Lyimo ambae ni mtoto wa kike ambae ameamua kujitoa na kufanya kazi hiyo ambayo imekuwa ikiachiwa watoto wa kike amesema kuwa ameweza kujikwamua kimaosha kwa kufanya mambo mengi ya maendeleo kama kulipa kodi ya nyumba na matumizi mengine madogo madogo

Nae Mkurugenzi wa UPTOWN CARWASH Joachim Mushi amesema kuwa lengo la kufungua hiyo ni ili kuweza kuwapa vijana ajira na aweze kuifikia jamii kwa urahisi kwa kuwa huduma hiyo ni muhimu na inaweza kuleta manufaa makubwa kwa vijanaInsert mkurugenzi.

Amesema licha ya kufungua fursa hiyo lakini bado kuna changamoto wanazokabiliana nazo zikiwemo ushindani wa biashara hiyo kwa kuwa sehemu za kuoshea magari jijini Arusha zimekuwa ni nyingi na hivyo wateja kukosa kushindwa kujua ni sehemu gani ina ubora

Hata hivyo amewataka vijana wa kike kutochagua kazi na badala yake wajitume ikiwa ni pamoja na kufanya biashara mbalimbali za ujasiriamali ili waweze kujenga maisha yaliyo bora kwa sasa na badae

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu