Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea
eneo la Mkambalani wilayani Morogoro, ikihusisha basi la
Happy Nation lenye namba za usajili T 702 DGF likilokuwa
linatokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na lori la mizigo
lililokuwa linatoka Zambia kwenda Dar es Salaam.
Ajali hiyo imetokea leo Julai 20, 2022 majira ya saa 3:00
asuhubi, ambapo baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo
wamesema kuwa kilichosababisha ni kutozingatiwa kwa sheria
za barabarani,wakiomba jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani kuongeza umakini ili kupunguza ajali zisizo za
lazima.
Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Morogoro ACP Ralph Meela,
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo chanzo cha ajali
kinadaiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa basi hilo ambaye
alikuwa akijaribu kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari
na kusababisha ajali.
