Wapiganaji wa kundi la al-Shabab lenye misimamo mikali ya Kiislamu, waliokuwa wamejihami kwa sialha nzito wameivmia kambi ya kijeshi ya jimbo la Puntland hapo jana, na kuwauwa watu wapatao 70 na kujeruhi wengine kadhaa.
Maafisa wamesema ni shambulio baya kuwahi kutokea katika jimbo hilo kwa miaka kadhaa.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wanamgambo wa kundi hilo walipouvamia na kuukamata mji wa Af Urur.
Gavana wa jimbo la Gari Yusuf Mohamed ameliambia shirika la habari l Reuters kwamba jeshi la Puntland limeukamata tena mji huo.
Wakazi wa eneo hilo wameripoti kushuhudia machafuko hayo, wakielezea namna wapiganaji wa al-Shabab walivyo wakata vichwa baadhi ya raia wa eneo hilo.
