Wapinzani nchini Senegal wamelalamika juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo

Wapinzani nchini Senegal wamelalamika juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo.

Uchaguzi huo uligubikwa na mivutano na kabla ya kufanyika ulikumbwa na ghasia.

Senegal ni nchi inayojulikana kuwa ya amani na demokrasia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi vituo 147 vya kupigia kura viliharibiwa.

Polisi pia wameeleza kuwa watu watatu wametiwa ndani. Aliyekuwa rais wa Senegal Abdoulaye Wade amemlaumu rais wa sasa Macky Sall kwa kuchochea matatizo katika uchaguzi huo ili kuzuia ushindi wa upinzani.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutolewa mapema leo. Zaidi ya watu milioni 6.2 waliandikishwa kupiga kura nchini Senegal.

Exit mobile version