Wasafirishaji wa wahamiaji haramu kutaifishiwa mali zao.

KAMANDA wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna amesema kuanzia sasa watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji hao  kwani navyo vitataifishwa .

Akizungumzia hatua walizozichukua kwa wahamiaji haramu 72 waliokamatwa mapema wiki hii,kamanda Shanna alisema kushiriki kwenye biashara hiyo ni kosa la kubwa la kijinai.

Amesema wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji fedha na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.

Kamanda Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za wale watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.

Aidha amesema sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini hivyo itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa adhabu zote na kufungwa .

 

 

 

Exit mobile version