Washukiwa watano wa tawi la kigaidi la Al-Qaeda nchini Yemen wameuawa jumapili katika kile kinachoelezwa na mamlaka kuwa shambulizi la anga lililotekelezwa na ndege za Marekani mashariki mwa jiji la Sanaa.
Shambulizi la mapema jumapili lililenga gari lililokuwa likisafirisha silaha katikati mwa jimbo la Marib kutoka Yakla jimboni Baida,kwa mujibu wa jeshi.
Maafisa wamesema gari lilikuwa linamilikiwa na kiongozi mmoja wa Al-Qaeda katika ghuba ya kiarabu ambayo Marekani inalitaja kuwa tawi hatari zaidi lenye msimamo mkali.
Shambulizi la jumapili linakija ikiwa ni masaa 24 kupita baada ya kutekelezwa shambulizi kama hilo lililoua wanamgambo 3 kusini mwa jimbo la Shabwa ambalo limelengwa zaidi na vikosi vya Marekani.
