Wasiopeleka michango ya wafanyakazi NSSF kukiona.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi,
Vijana na Ajira Mhe Anthony Mavunde ameagiza kukamatwa
kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Knight Support ambayo ni
mwajiri mdaiwa sugu.


Agizo hilo amelitoa baada ya kuongoza kikao kati ya Serikali
kupitia Wizara yake, uongozi wa NSSF na Kampuni hiyo,
kufuatia malalamiko ya wafanyakazi kukatwa makato lakini
hayapelekwi katika mfuko wa hifadhi NSSF.



Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa NSSF William Erio,
amesema kampuni hiyo iliacha kupeleka makato hayo toka
mwaka 2011, jambo lililowalazimu kufungulia kesi mahakamani
dhidi ya kampuni hiyo mwaka 2018.

Exit mobile version