Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam Omary Kumbi
la moto, amewataka wafanyabiashara wote katika Machinjio ya
Vingunguti kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa
afya katika kipindi hiki cha janga la Corona.
Maelekezo hayo yanayopaswa kufuatwa ni pamoja na kunawa
mikono, kuvaa barakoa na kuepusha misongamano isiyokua ya
lazima.
Meya Omary Kumbi amesisitiza kuwa yoyote atakayekiuka
agizo hilo la kuvaa barakoa katika Machinjio ya Vingunguti
watashikwa na polisi na kuwekwa ndani.
