Wastani wa wanafunzi saba hupewa ujauzito kila mwezi katika wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro

In Kitaifa

Wastani wa wanafunzi saba hupewa ujauzito kila mwezi katika wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, jambo ambalo linatishia mustakabali wa elimu ya mtoto wa kike wilayani humo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Agnes Hokororo hadi kufikia Juni mwaka huu jumla ya wanafunzi 42 wa shule za msingi na sekondari wamekatisha masomo baada ya kupata ujauzito.

Takwimu hizo zimetajwa ni kwa kipindi hadi kufikia shule hizo zinafungwa mwezi mmoja uliopita ambapo mipango imewekwa kufanyiwa tena kwa vipimo kwa wanafunzi wote wa kike mara baada ya kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari Julai 3 mwaka huu.

Amesema pamoja na mimba za utotoni lakini pia katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu kumeripotiwa matukio 25 ya ubakaji na nane ya ulawiti, jambo ambalo linaashiria wananchi kukiuka utii wa sheria

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu