Watafiti wagundua kwa nini mtu huchelewa kulala au kutopata usingizi ugenini.

Inawezekana wewe ni mmoja kati wa watu ambao hukosa usingizi kabisa au kushindwa kulala vizuri pindi unapotembelea sehemu tofauti na uliyoizoea.

Yawezekana ikawa ugenini, hotelini au sehemu nyingine na unajiuliza ni kwa sababu ipi inakufanya uchelewe kulala au kutolala kabisa.

Sasa leo wanasayansi wameelezea kuhusu swala hilo, ambapo wakisema husababishwa na ubongo.

Wamesema mtu anapolala ugenini au mahala asipopazoea,nusu ya ubongo wake ndiyo hulala, lakini nusu nyingine inakuwa ‘active’ na hii ni kutokana na mabadiliko ya mazingira.

Unaambiwa jambo hili hupelekea mtu kuchelewa kupata usingizi na huwahi kuamka pengine isivyo kawaida.

Wakati mwingine awapo katikati ya usingizi huweza kushtuka anaposikia milio ya vitu kama ndege, mtu anatembea na vitu vingine vingi.

Exit mobile version