Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni leo
amezunguza na wanahabari na kutoa taarifa ya kukamtwa kwa
watuhumiwa 3 kuhusiana na tukio la kuchoma moto Ofisi za
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tarehe 14
mwezi wa nane 2020 katika Kata ya Kimandolu, Tarafa ya Suye
na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
ACP Salum Hamduni amesema kuwa Mara baada ya tukio hilo
kutokea uchunguzi wa kina ulifanyika kuwabaini na
kuwakatama watu wote waliohusika katika tukio hilo ambapo
tarehe 19.08.2020 alikamatwa mlinzi wa Ofisi hiyo aitwaye
Deogratius Augustino Malya.
Mtaa wa Mastory tunamsogeza kwako Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni,umsikie alivyokuwa
akitoa taarifa hiyo mapema hii leo.
