Watoto wa Mfalme wakamatwa Saudia.

Mawaziri 11 miongoni mwao wakiwa ni wana wa ufalme wameachishwa kazi na hata kuzuiliwa katika Mabadiliko makubwa yaliyotangazwa kwenye serikali ya Saudia.

Wengine wanaozuiliwa ni mawaziri wa zamani ambao wamehusishwa na kashfa za rushwa.

Katika hatua hiyo ambayo si ya kawaida inaelekea mwana mrithi wa mfalme Mohammed Bin Salman ambaye ndiye anaesimamia kitengo cha kupambana na ufisadi, anapania kujitenga na kuwadhibiti wapinzani wake wenye mamlaka makubwa nchini humo.

Miongoni mwa wanazuiliwa ni wana wa wafalme mmojawao ni mtoto wa marehemu mfalme Abdullah Prince Miteb aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kikosi cha kiusalama National guard ambapo sasa amepokonywa wadhfa huo.

Mwengine ni billionaire Prince Al-Waleed bin Talal.

Inaripotiwa kwamba hisa katika kampuni aliyoekeza huko uingereza iitwayo Kingdom Holding, zimeporomoka kutokana na hisia hizo.

Exit mobile version