Watoto watatu walionusurika kwenye Ajali ya basi la wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent, ambayo ilipoteza maisha ya wanafunzi 32, wanatarajia kurejea nchini August 18, 2017 baada ya kupatiwa matibabu nchini Marekani.
Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa mstari wa mbele kusimamia shughuli ya kuwasafirisha, amesema ratiba ya mapokezi itaanza mapema zaidi ambapo itakuwa saa Moja asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, ‘KIA’ ambapo Makamu wa Rais Samia Sulu Hassan atawaongoza Watanzania.
Aidha nyalandu amesema ku wa wananchi na familia wanatarajiwa kufika uwanjani hapo mapema kidogo ikiwa ni pamoja na viongozi mbali mbali wanatarajiwa kushiriki Mapokezi hayo.
