Kiasi ya watu 1,000 wameandamana hapo jana mjini Moscow kupinga hatua ya serikali kudhibiti matumizi ya mtandao wa Intaneti.
Urusi katika miaka ya hivi karibuni imekua ikichukua hatua za kudhibiti matumizi ya Intaneti pamoja na kuwafungulia mashitaka watu kadhaa kwa makosa yanayohusiana na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Waandamanji walisikika wakipaza sauti kupinga hatua hiyo na polisi nchini humo wanasema kiasi ya watu 800 walishiriki maandamano hayo yaliyoandaliwa na chama cha upinzani kilichokuwa kikiongozwa na Waziri Mkuu wazamani Mikhail Kasyanov.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP amekadiria watu waliojitokeza kwenye maandamano hayo kuwa kati ya 1,000 na 1,500.
Tangu Januari mosi makampuni ya intaneti nchini humo yametakiwa kutunza ujumbe wa mawasiliano binafsi kwa ajili ya kuwasilisha katika vyombo vya serikali pindi utakapohitajika.
