Watu 26 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha, aliyewafyatulia risasi waumini katika kanisa moja lililopo jimbo la Texas nchini Marekani wakati wa ibada iliyofanyika jana.
Gavana wa jimbo hilo Greg Abbott amethibitisha idadi ya watu waliofariki na kusema kuwa, hilo ni tukio baya zaidi la mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya Texas.
Aidha Rais Donald Trump ambaye yuko ziarani Asia amesema kuwa, tukio la shambulizi hilo halivumiliki na Wamarekani wanatakiwa kupinga kila kitu kinachihusiana na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.
