Watu tisa wakutwa wamekufa ndani ya lori huko Texas

Watu tisa wamekutwa wamekufa ndani ya lori lilokuwa limeegeshwa nje ya eneo la maduka katika jimbo la Texas nchini Marekani.
Maafisa nchini humo wamelielezea tukio hilo kama kushindwa kwa jaribio la wasafirishaji haramu wa binadamu katika juhudi zao za kuingiza watu nchini humo kwa kutumia njia zisizo halali.
 Dereva wa lori hilo ametiwa mbaroni na karibu watu wengine 20 walio okolewa ndani ya lori hilo wamepelekwa hospitali kutokana na hali zao kiafya kuwa mbaya.
Maafisa waliitwa kwenda katika eneo lilipokuwa limeegeshwa lori hilo na kukuta tayari watu wanane kati ya waliokuwemo ndani yake wakiwa tayari wamefariki dunia.
Exit mobile version