Watu zaidi 50 wauawa kwa shambulio la Boko Haram.

Idadi ya vifo inayotokana na shambulio la kundi la Boko Haram dhidi ya timu ya utafutaji wa mafuta kaskazini mashariki mwa Nigeria mapema wiki hii imeongezeka hadi kufika watu zaidi ya 50.

Likinukuu vyazo vya kijeshi, kitabibu na makundi ya kutoa misaada ya kiutu, shirika la habari la Kifaransa la AFP limesema idadi ya vifo ni kubwa kuliko ile iliyotolewa na maafisa wa serikali, na kwamba maiti bado zinaendele kuwasili katika kitio cha afya.

Shambulio hilo la Jumatano iliyopita lililenga timu ya Shirika la Petroli la Kitaifa la Nigeria na wanajiolojia waliokuwa katika eneo la Ziwa Chad. Hapo jana, jeshi la Nijeria limesema kwamba watu watano kutoka katika kundi hilo wameuwawa, pamoja na wanajeshi kadhaa.

Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria kwa miaka minane sasa limekuwa likishambuliwa na uasi wa kundi la misiamamo mikali ya kidini la Boko Haram,ambalo limesababisha vifo vya watu 20,000 na wengine milioni 2.7 kuyahama makaazi yao.

 

Exit mobile version