Jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani linashirikana na chuo cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING kuendelea na kampeni ya kuhamasisha watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu kuzingatia alama na sheria za barabarani ili kuweza kupunguza ajali
Akizungumza na vyombo vya habari Mkufunzi kutoka taasisis ya Wide John Luganga amesema kuwa, kampeni hiyo imekuja mara baada ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la ajali za barabarani zinasosababishwa na uzembe jambo ambalo linapoteza nguvu kazi ya taifa
Amesema kuwa, kampeni hiyo wanaitoa kwa kila mkoa ambapo watazunguka nchi nzima na wanashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha wanaifikia jamii na watumiaji wa barabara elf kumi na mbili wameshapatiwa elimu hivyo itakuwa na matunda mazuri
Hata hivyo amewataka watanzania kuzingatia alama za barabarani na kuwataka madereva kwenda darasani ili kupata mafunzo ya udereva kwani hii ni njia mojawapo ya kuwa na nguvu kazi ya taifa
“Usiendeshe ukiwa umelewa, usiendeshe mwendo kasi mjini, na hakikisha unaheshimu vivuko vya watembea kwa miguu na ishara za alama barabarani “Amesema Mkufunzi.
Aidha amesema kuwa, magari ya kujifunzia yapo yanapatikana chuoni hapi ambapo kuanzia siku ya jumatatu jioni katika kanisa la KKKT usharika wa Salehe lililopo mtaa wa Levolosi Mkoani Arusha.
Amesema faida ya kuwa na cheti kwa madereva itasaidia kupata leseni kwa urahisi na cheti kitasaidia kupata kazi ya udereva popote na kurudisha leseni iliyokwisha muda wake
