watumishi 134 wa Hospitali ya Muhimbili wabainika kuwa na vyeti vya kugushi.

In Kitaifa

Watumishi 134 wa hospitali ya taifa Muhimbili wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi ,vya ngazi ya elimu ya sekondari hapa nchini.

Taarifa kutoka kwenye uongozi wa hospitali hiyo imesema , hospitali iliendesha zoezi la uhakiki wa vyeti vya elimu vya sekondari kwa watumishi wake, kwa kushirikiana na baraza la mitihani la Tanzania (NECTA) ,baada ya Agizo la serikali kutaka uhakiki ufanyike kwa watumishi wa Umma.

Idara iliyoathirika zaidi ni idara ya uuguzi ambapo watumishi wake takriban 70 ,wamekutwa na vyeti vya kughushi.

Baadhi ya idara nyingine zilizoguswa kwenye zoezi hilo ni Idara ya tiba watumishi 20, tiba shirikishi watumishi 14, upasuaji watumishi wanne, Idara ya Tehama watumishi 11, rasilimali, ufundi, fedha na mipango.

Kutokana na dosari hizo, uongozi huo umesema watumishi waliobainika wamekosa sifa za kuendelea kuwa watumishi wa umma, hivyo wametakiwa kujiondoa wenyewe kazini kabla ya tarehe 15 mwezi Mei mwaka 2017 ,ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.

Uongozi wa Muhimbili umetoa orodha ya watumishi walioghushi vyeti na kuwataka wakuu wa Idara mbalimbali, kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanaohusika hawaendelei kutoa huduma hospitalini hapo.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu