Watumishi 450 kati ya 1050 washinda rufaa ya vyeti feki,Serikali yatangaza

In Kitaifa

SERIKALI imetangaza kuwa watumishi wa umma 450 wameshinda rufaa, kati ya waombaji 1,050 ambao waliwasilisha rufaa zao katika mamlaka husika baada ya kutajwa katika orodha ya watumishi wenye vyeti feki.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro, amesema serikali iliendesha uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu ambako watumishi wa umma elfu tisa 9,932 walibainika kukutwa na vyeti feki.

Dk Ndumbaro amesema baada ya kutangazwa kwa orodha hiyo ya watumishi wenye vyeti feki, watumishi elfu moja 1,050 walikata rufaa na watumishi 450 pekee, walishinda rufaa hizo huku watumishi 8,800 wakiridhika na matokeo hayo.

Ndumbaro amesema  kuwa rufaa hizo zilizokubaliwa ni kwa watumishi wale waliokuwa wakitumia majina ya waume zao baada ya kuolewa, ambayo yalitofautiana na majina yaliyopo kwenye vyeti na baada ya uhakiki walionekana kama ni vyeti feki.

Aidha, amefafanua kuwa wengine walioshinda rufaa ni wale ambao majina yao ya kidato cha nne yalikuwa tofauti na majina ya kidato cha sita kwa kuwa kidato cha nne hakutumia jina la kati kama kidato cha sita, lakini baada ya kujieleza, wamekubaliwa rufaa na kurejeshwa katika utumishi wa umma.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu