Wazazi Kilimanjaro hawana ushirikiano kwa mabinti wanaopata mimba.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu, amesema wazazi wa Mkoa wa Kilimanjaro hawaonyeshi ushirikiano kwa mabinti zao wanapopata ujauzito.

Buswelu amesema jukumu la wazazi ni kuwalea watoto wao kwa weledi, ili wafikie malengo yao ya maisha kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Amesema hayo wakati wa mahafali ya kidato cha nne, katika Shule ya Sekondari ya ALCP ­Kilasara iliyopo mjini humo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Revocatus Mbuya, amesema shule hiyo ilipoanza mwaka 2012 ilikuwa na wanafunzi 106, lakini 91 ndiyo walioweza kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

Exit mobile version