Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu na kutowaruhusu wanafunzi kushiriki kwenye sherehe za usiku lakini pia kukenea utoro katika baadhi ya shule zinazopatikana ndani ya kata hiyo.

Hayo ameyaeleza akiwa katika ziara zake za kupitia na kukagua hali ya taaluma katika kata hiyo na kugundua kuwepo kwa utoro na wazazi kutosimamia suala la elimu kwa watoto wao hali inayoweza kupelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Ziara hiyo inalenga kutatua changamoto zilizopo katika suala la elimu kata ya Itagano ilyopo Tarafa ya Sisimba na kuzungumza na watumishi waliopo katika kata hiyo.

Exit mobile version