Waziri Kairuki -Tupinge ukatili wa kijinsia.

In Kitaifa

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amewataka Watanzania kutumia nguvu zao katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Waziri wa Nishati, Angellah Kairuki akiwaasa wadau na watanzania kujikita katika kupambana na ukatili wa kijinsia wakati akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba.

Waziri Kairuki ameyasema hayo alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kimsingi kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na dunia bado ni kubwa na kwa mujibu wa Taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Ameongeza kuwa takwimu zinonesha kuwa asilimia 42 ya wanawake waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa wenza wao ama wa kimwili,au ukatili unaohusisha ngono.

“Nawaomba watanzania wenzangu katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto” alisema Mhe. Angellah.

Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa athari za ukatili wa kijinsia ni kubwa sana katika Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa kampeni hii ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hasa ilenge kuinua uelewa wa jamii na wadau mbalimbali kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Kampeni hii imekuja wakati muafaka na kwakuwa tatizo la ukatili wa kijinsia hapa nchini bado ni kubwa basi itasaidia kulitatua kwa jitihada za pamoja za Wadau na Serikali” alisema Mhe. Dkt. Ndugulile.

Naye Mkurugenzi wa WILDAF Tanzania Dkt. Judith Odunga ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wao katika kupambana na ukatili wa kijinsia na kuomba kufanyiwa kwa marekebisho ya baadhi ya Sheria ili ziende sambamba na kupinga ukatili wa kijinsia nchini.

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 na kwa mwaka 2017 Kauli mbiu inasema FUNGUKA! Ukatili Dhidi ya wanawake na Watoto haumwachi Mtu Salama: CHUKUA HATUA!

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu