Waziri Lukuvi amjibu Sumaye.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi, amesema mtu yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na kuendeleza ardhi hiyo, ni sababu tosha ya kunyang’anywa.

Waziri Lukuvi amebainisha hayo ikiwa imepita siku moja toka aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye, kudai chanzo cha kupokonywa shamba lake ni siasa tu za yeye kuhama chama cha CCM.

 

Kuhusu mashamba na viwanja kuchukuliwa Waziri Lukuvi amesema kuwa, kila mtu atambue iwe ni kiwanja au shamba kama unatabia ya kutolipa kodi ya ardhi, ni sababu tosha kunyang’anywa shamba lako au ardhi unayomiliki.

 

Waziri Lukuvi amesema imejitokeza kwa watu wachache kuchukua ardhi kubwa kwa miaka mingi kuliko hata uwiano wa uendelezaji wa ardhi hiyo.

 

Kwa upande mwingine Waziri Lukuvi amesema kuwa, serikali imekuwa na huruma kwa miaka mingi kwa wananchi wake, lakini serikali ya uongozi huu wamekubaliana kila mtu afuate sheria anazo paswa kuzifuata.

Exit mobile version