Waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa,jana
alifanya mkutano maalaum katika Wilya ya Mkuranga ambapo
amebaini mambo kadhaa,likiwemo la watumishi wa serikali
hasiokaa Mkuranga na badala yake wanatokea Dar es salaama
kila siku.
Kufuatia hilo ametoa muda mpaka kufikia tarehe 30 mwezi 12
watumishi hao wote wawe wamehamia katika maeneo yao ya
kazi,wakiwemo watumishi wa Uhamiaji,Nida,Afisa Tarafa na
watumishi walio kwenye kamati ya ulinzi na Usalama.
