WAZIRI Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania KASSIMU MAJALIWA amewataka wakuu wa Wilaya Nchini ,kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wote ambao wanashindwa kuzingatia sheria za utumishi, kwa kuvujisha taarifa mbalimbali za Serikali.
Amesema ni wazi kuwa jambo lolote la ndani la serikali au nyaraka zozote za serikali hazipaswi kusikika nje, ambapo kutokana na kuwepo kwa tabia ya kuvujisha taarifa hizo wakuu wa wilaya wanatakiwa kuchuka hatua mara moja, ili kukomesha tabia hiyo.
Hayo yamesemwa waziri mkuu MAJALIWA wakatia Akizindua Program ya Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi, kutoka katika Mkoa 6 hapa nchini ambayo yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa katika kipindi hiki cha utandawazi suala la utunzaji wa taarifa za serikali bila kuvuja pamoja na matumzi mazuri ya nyaraka ni muhimu kuzingatiwa.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya za mikoa 6 walioshiriki katika mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma CHRISTINA MDEME, amesema kuwa wao kama viongozi wako tayari kufanya kazi wakati wowote iwe usiku, mchana, kiangazi au masika bila kujali mazingira ya kazi.
