Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa, leo Juni 23 amefika katika hifadhi ya Ngorongoro
mkoani Arusha,kuzungumza na wakazi wa eneo hilo
waliokubali kuhama kwa hiari yao.
Waziri mkuu ameongozana na viongozi mbali mbali akiwemo
Waziri wa Elimu,Waziri wa Mifugo pamoja na Waziri wa maji
Mh Jumaa Aweso,ambaye amezungumza na kusema miundo
mbinu ya upatikanaji wa maji katika eneo ambalo wakaaazi hao
wanahamia pale mkoani Tanga kuwa ipo tayari.
Kwa upande wake Mhe Waziri Mkuu Majali akizungumza na
wananchi hao amesema kuwa,Serikali iko bega kwa bega nao
katika kuhakikisha wanafika salama katika makazi yao mapya,
na kupata huduma zote muhimu.