Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini ,waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini ,waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo ,katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa 24 kuwa Kamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo Mei 25, mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu,Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

Exit mobile version