Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mamlaka mbalimbali
nchini kuheshimuwa hukumu halali zitolewazo na mahakamani
na iwapo kuna asiyekubaliana na mamuzi hayo, ni vema kukata
rufaa na siyo kushindwa kutekeleza.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Mei 11, 2023 bungeni
katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo ambapo Mbunge
wa Ushetu Emmanuel Cherehani (CCM), ametaka kujua kauli
ya Serikali kuhusu Mamlaka za Hifadhi kushindwa kurudishia
mifugo kwa wafugaji ambao wameshinda kesi.
Mbunge huyo amesema kumekuwa na kilio kikubwa kutoka
kwa wafugaji ambao walishinda kesi zao na mahakamani
ikaamuru warejeshewe mifugo yao lakini kumekuwa na
ukimywa wa muda mrefu kwa mamlaka hizo kutekeleza
maagizo hayo halali ya mahakama.
Lakini pia Waziri Mkuu Majaliwa akatoa majibu ya swali
lililoulizwa na mbunge wa Chake chake Ramadhani Seleman
Ramadhani,juu ya tetesi za ubalozi wa Denmark kutaka
kufungwa Tanzania.
