Waziri mkuu wa India Narendra Modi, amewasili nchini Israel na kuwa waziri wa kwanza kwa India kufanya ziara nchini humo.
Bwana Modi ambaye alisema India na Israel zina uhusiano wa miaka mingi, anatarajia kusaini makubaliano ya kijeshi na usalam wa mitandao.
Bwana Modi hatasafiri kuenda Ramallah au kukutana na viongozi wa Palestina, kama ambvyo wageni wengine hufanya.
Ziara hiyo inaonekana kuwa mabadiliko makubwa, kwa msimamo wa India kwa taifa la Israel.
